Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai
Radio China Kimataifa


Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai ni moja ya vyuo vikuu muhimu nchini China, kilianzishwa mwaka 1896. Hivi sasa chuo kikuu hicho kina vitivo 21 vya uhandisi wa meli na upashanaji bahari, uhandisi wa mashine na nishati na kadhalika, vina kozi 55 kama vile sayansi, uhandisi, utamaduni, usimamizi, kilimo, uchumi, sheria na elimu. Kinakaribia kiwango cha kwanza duniani katika elimu kadhaa kama vile mawasiliano ya simu na upashanaji habari, uhandisi wa meli na bahari, udhibiti unaojiendesha, nyenzo zinazochanganywa na kadhalika.

Hivi sasa, chuo kikuu hicho kina wanafunzi elfu 14 wa shahada ya kwanza, wanafunzi zaidi ya 7000 wa shahada ya pili na ya udaktari na wanafunzi zaidi ya 1600 kutoka nchi za nje. Katika miaka mingi iliyopita, Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Shanghai kimewaandaa wasomi zaidi ya laki moja ambao ni pamoja na wanasiasa, wanaharakati wa mambo ya kijamii, wanaviwanda, wanasayansi, maprofesa na wataalamu. Ukitaka kufahamu habari nyingi zaidi kuhusu Chuo Kikuu Cha Mawasiliano Cha Shanghai, soma tovuti ifuatayo:http://www.sjtu.edu.cn/