Wanafunzi wa Ng'ambo Nchini China
Radio China Kimataifa

Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa China unaongezeka kwa haraka, na hadhi ya China duniani inainuka siku hadi siku, na kuwavutia vijana wengi zaidi wa nchi za nje kuja kusoma nchini China. Hivi sasa, wanafunzi elfu 77 kutoka nchi mbalimbali duniani wanasoma nchini China, ambapo asilimia 90 kati yao wanafunzi wanajilipia wenyewe. Wanafunzi hao wanatoka nchi na sehemu zaidi ya 170 kama vile Korea ya Kusini, Japan, Marekani, Vietnam, Indonesia, Thailand, Ujerumani, Russia, Nepal, Ufaransa, Australia na Malaysia.

Kozi ambazo wanafunzi wa ng'ambo wanaosomea ni Kichina, utamaduni wa China, historia ya China, na utibabu wa Kichina. Katika miaka ya hivi karibuni baadhi ya wanafunzi pia wameanza kusomea kozi za sheria, mambo ya fedha na uchumi, uhasibu na kozi nyingine za kisayansi.

China inachukua hatua mbalimbali za kuongeza wanafunzi wa ng'ambo, kwa mfano kuwaruhusu wanafunzi wa ng'ambo kuishi nje ya shule ili waweze kuingiliana na wakazi wa China, na kufahamu zaidi mambo ya China; kutoa mihadhara kwa lugha za Kichina na Kiingereza kwa wanafunzi wa shahada ya pili, ili kuwavutia wanafunzi wasiojua sana lugha ya Kichina.

Kutokana na takwimu zisizokamilika, tangu kuasisiwa kwa China mpya hadi leo, idadi ya wanafunzi wa ng'ambo waliosoma nchini China imezidi laki 6 na elfu 30 kutoka nchi na sehemu 170 duniani. Wanafunzi hao wanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi zao, na kuhimiza maingiliano na ushirikiano kati ya nchi zao na China.