Kujifunza Kichina
Radio China Kimataifa

Kujifunza Kichina ni lengo la wanafunzi wengi la kuja China kwa mafunzo. Hivi sasa asilimia 60 ya wanafunzi wa ng'ambo nchini China wanajifunza Kichina. Kipindi cha kujifunza Kichina hakina muda maalum, kuna darasa la kipindi cha miezi kadhaa au wiki kadhaa, pia kuna elimu ya Kichina ya shahada ya kwanza ya miaka minne. China imetunga vitabu vya aina mbalimbali vya kiada kwa ajili ya wanafunzi wa ng'ambo, walimu wanatoa mafunzo kwa lugha mbili za Kichina na Kiingereza au kwa Kichina pekee kutokana na kiwango tofauti cha wanafunzi.

Hivi sasa vyuo vikuu zaidi ya 300 vya China vinaweza kupokea na kufundisha wanafunzi wa ng'ambo Kichina, wanafunzi wanaotaka kusoma nchini China wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na vyuo hivyo.

Kuanzia mwaka 1992, China ilianzisha mtihani wa kiwango cha lugha ya Kichina unaofanana na TOEFL kwenye lugha ya Kiingereza. Hivi sasa China imeweka vituo vya mtihani wa aina hiyo katika nchi na sehemu 28 duniani.