Kusoma Katika Chuo Kikuu Nchini China
Radio China Kimataifa

Wanafunzi wakitaka kusoma katika vyuo vikuu nchini China wanatakiwa kuwa na shahada husika na kiwango fulani cha lugha ya Kichina, baadhi ya vyuo vikuu pia vitawapa mtihani maalum kabla ya kuwaandikisha. Wanafunzi wa nchi za nje wanaweza kuwasiliana na vyuo vikuu vya China kwa kupitia mtandao, wakiandikishwa, watarahisishwa urasmu wa kuja China. Hivi sasa vyuo vikuu zaidi ya 300 nchini China vinawaandikisha wanafunzi wa nchi za nje.

Gharama za shule nchini China ni za chini, na inatofautiana kati ya vyuo tofauti, hivi sasa karo ya mwaka mmoja ni kiasi cha yuan elfu 20 kwa wastani.

China inazingatia sana kupata wanafunzi wa ng'ambo kusomea elimu ya juu , na kulifanya jambo hilo kama njia muhimu ya kuinua hadhi yake ya kimataifa katika eneo la elimu, na kuvifanya vyuo vikuu viwe vya daraja la kwanza duniani. China itaendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira, ili kuwavutia wanafunzi wengi zaidi wa ng'ambo, hasa wanafunzi wa shahada ya pili.