Mipango ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ya Taifa ya China
中国国际广播电台

Mpango wa Utafiti wa Kimsingi

Mpango wa utafiti wa kimsingi ulianza kutekelezwa mwezi wa Machi mwaka 1997, mpango huo pia unaitwa mpango wa “973”.

Mpango wa “973” unahusu kilimo, nishati, upashanaji habari, maliasili, mazingira, idadi ya watu na afya na nyenzo.

Katika miaka ya karibuni, serikali imetenga fedha yuan milioni mia kadhaa kwa ajili ya mpango huo na imeanzisha miradi zaidi ya 300, na baadhi ya miradi iliyoanzishwa mapema imepata mafanikio.

Mpango wa Utafiti wa Sayansi na Teknolojia ya Juu

Mpango huo ulitolewa na wanasayansi wakubwa wanne wa China katika mwezi Machi mwaka 1986, kwa hiyo mpango huo pia unaitwa mpango wa “863”.

Mpango wa “863” umechagua miradi 15 ya utafiti wa viumbe, anga ya juu, upashanaji habari, laser, mfumo unaojiendesha, nishati, nyenzo mpya n.k.

Ili kutekeleza mpango huo wa “863” vituo vingi vya utafiti wa sayansi na teknolojia ya juu vimeanzishwa, na vimeandaa wanasayansi wengi vijana, mafanikio mengi yenye kiwango cha kimataifa yamepatikana.

Mpango wa Kuendeleza Sayansi na Teknolojia ya Kilimo

Mpango huo wa sayansi na teknolojia ya kilimo pia unaitwa “mpango wa cheche za moto”. Neno “cheche za moto” linatokana na usemi wa Kichina “cheche za moto zaweza kuunguza mbuga kubwa”, ikimaanisha kuwa sayansi na teknolojia ya kilimo vinaweza kuenea haraka kote nchini China.

Mpango huo ulianza kutekelezwa mwaka 1986. lengo la mpango huo ni kuvumbua teknolojia mpya ya kilimo na kuieneza vijijini na kuwaelimisha wakulima watumie teknolojia mpya kuendeleza kilimo.

Katika miaka zaidi ya kumi tokea mpango huo uanze kutekelezwa wataalamu wa kilimo wamevumbua teknolojia nyingi na kwa kiasi kikubwa wameendeleza kilimo. Mwaka 2003 wataalamu wa kilimo waliotesha aina zaidi 300 za mbegu bora na kutumika katika hekta milioni 10, na walitoa njia mpya ya umwagiliaji ambayo inaokoa maji kwa 30%.

“Mpango wa cheche za moto” umesukuma uzalishaji wa aina moja ya kilimo kwa kiwango kikubwa na wa kisasa, umeongeza mapato ya wakulima na kuwafahamisha kuwa teknolojia ndio mali. Watu wa nchi za nje wanasema “mpango wa cheche za moto” ni mpango wa kuwaendeleza wakulima.

Mpango wa kueneza matokeo ya teknolojia mpya za hali ya juu

Mpango wa mwenge” yaani mpango wa China wa kueneza matokeo ya teknolojia mpya za hali ya juu ni mpango wa kuelekeza katika kuendeleza shughuli za teknolojia mpya za hali ya juu. Mpango huu unalenga kuenzi nguvu bora za sayansi na teknolojia za China, kuhimiza matokeo ya teknolojia mpya za hali ya juu yatumiwe katika kuzalisha bidhaa na kuzifanya bidhaa hizo ziingie kwenye soko la nchini na duniani. Mpango huu ulitekelezwa kuanzia mwaka 1988. Sekta muhimu za kuendeleza teknolojia mpya za hali ya juu ni kama vile elektroniki na upashanaji habari, teknolojia za viumbe, nyenzo mpya, nishati mpya, kubana matumizi ya nishati na kujipatia ufanisi wa juu na kuhifadhi mazingira.

Hivi sasa China imeanzisha sehemu 53 za kitaifa za maendeleo ya teknolojia mpya za hali ya juu. Toka mwaka 1991 hadi hivi sasa, wastani wa ongezeko la malengo muhimu ya uchumi wa sehemu hizo unafikia asilimia 40 kwa mwaka. Sehemu hizo zimekuwa nguzo za kusukuma mbele maendeleo ya teknolojia mpya za hali ya juu na kuboresha miundo ya uchumi wa taifa.

Mwaka 2004, mapato ya sehemu 53 za maendeleo ya teknolojia mpya za hali ya juu yalizidi renminbi yuan trilioni 2, sehemu kadha wa kadha maarufu miongoni mwa sehemu hizo kama vile Sehemu ya sayansi na teknolojia ya Zhongguanchun ya Beijing na Sehemu ya teknolojia mpya ya hali ya juu ya Shanghai, mapato yao ya mwaka 2004 yalizidi yuan bilioni 150. Na katika sehemu hizo pia zimeanzishwa kwa mashirika mengi ya shughuli za teknolojia mpya za hali ya juu kama vile Kampuni ya kompyuta ya Lenovo, Kampuni ya kompyuta ya Fonder, makampuni ya upashanaji habari ya Huawei na Datang.

Mpango wa China wa chombo cha safari ya anga ya juu ya kubeba binadamu

Mpango huo umetekelezwa kuanzia mwaka 1992. Mpango huo unatekelezwa kwa hatua tatu, ya kwanza ni kuwapeleka wanaanga wa China kwenye anga ya juu; ya pili ni kutatua teknolojia husika ili kurusha maabara ya anga ya juu yenye watu ambayo itawekwa kwenye anga ya juu kwa muda mfupi; ya tatu ni kujenga kituo kinachotunzwa na watu kwa muda mrefu ili kutatua masuala ya kufanya majaribio makubwa ya kisayansi na teknolojia ya matumizi kwenye anga ya juu.

Mwishoni mwa mwaka 1999 China ilifanikiwa kurusha na kurudisha Chombo cha Shenzhou No.1cha safari za anga ya juu. Katika zaidi ya miaka mitatu baada ya hapo, China ilifanya majaribio mara tatu ya kurusha chombo cha safari ya anga ya juu bila kubeba binadamu. Tarehe 15 Oktoba mwaka 2003 China ilirusha Chombo cha Shenzhou No.5 kilichobeba binadamu kwenye safari ya anga juu, Bwana Yang Liwei amekuwa mwanaanga wa kwanza wa China kwenye anga ya juu. Kufanikiwa kurushwa kwa Chombo cha Shenzhou No.5 kumeonesha kuwa China imekuwa nchi ya tatu duniani ikiifuata Russia na Marekani kuwa na uwezo wa kuanzisha shughuli za kubeba binadamu kwenye safari ya anga ya juu kwa kujitegemea.

Roketi zilizotumiwa katika kurusha vyombo vya safari ya anga ya juu vya China zilisanifiwa na kutengenezwa kwa ajili ya vyombo vya kubeba binadamu kwenye safari ya anga ya juu. Roketi ya Changzheng No.2 F ni roketi kubwa kabisa, ndefu kabisa na yenye miundo mingi ya utatanishi kabisa.

Habari zinasema kuwa, mwaka 2006 China itarusha chombo cha safari ya anga ya juu ya Shenzhou No.6, ambapo chombo hicho kitawabeba wanaanga kadhaa, na wanaanga hao huenda wataweza kutoka kwenye chombo na kutembea kwenye anga ya juu.

Mradi wa China wa kufanya utafiti kwenye mwezi

Mradi huo utatekelezwa kwa vipindi vitatu: Kwanza, kurusha satlaiti itakayouzunguka mwezi na kufanya utafiti wa mwezi; Pili, kukifanya chombo cha utafiti wa mwezi kitue kwenye ardhi ya mwezi ili wanaanga waweze kutembea na kufanya uchunguzi kwenye ardhi ya mwezi; tatu kukamilisha kazi ya chombo kutembea na kufanya uchunguzi kwenye ardhi ya mwezi na kurudisha chombo kwenye dunia. Hivi sasa kazi ya kipindi cha kwanza inafanyika.

Mradi wa kurusha satlaiti ya itakayouzunguka mwezi na kufanya utafiti umetekelezwa kuanzia mwezi Januari mwaka 2004, China itarusha satlaiti ya Chang'e No.1 kwa kufanya utafiti kwenye ardhi ya mwezi.

China imeendeleza shughuli za safari ya anga ya juu katika zaidi ya miaka 40 iliyopita, na imekuwa na uwezo wa kusanifu na kutengeneza yenyewe rekodi za uchukuzi na satlaiti, tena imesanifu na kutengeneza chombo cha safari ya anga ya juu, mwaka 2004 ilifanikiwa kurusha chombo cha kubeba mwanaanga kwenye safari ya anga ya juu. Lakini wanasayansi wa China wanaona kuwa, bado kuna matatizo mengi ya kiteknolojia katika kufanya utafiti wa mwezi.

Habari zinasema kuwa, hivi sasa China inafanya ukarabati wa mfumo wa upimaji na udhibiti wa upashanaji wa habari na mfumo wa ardhini katika mradi wa kurusha satlaiti ya China itakayorushwa ili kuuzunguka mwezi na kufanya utafiti wa mwezi, na kazi ya kusanifu na kutengeneza satlaiti na mfumo wa roketi kabla ya mwezi Oktoba mwaka 2006.