Idara za utafiti wa kisayansi na kiteknolojia za China
中国国际广播电台
Idara za utafiti wa kisayansi na kiteknolojia za China zimegawanyika katika aina mbili, zinazojiendesha au zinazoendeshwa chini ya vyuo vikuu au mashirka. Idara za utafiti wa kisayansi na kiteknolojia zinazojiendesha zinagharimiwa na serikali ya China, idara hizo zimefikia zaidi ya 2000 nchini China, miongoni mwake idara za ngazi ya kitaifa ni 500 hivi, na idara zinazoendeshwa na vyuo vikuu au mashirika ni nyingi zaidi.

Idara za utafiti wa kisayansi na kiteknolojia za China zinashughulikia utafiti wa kimsingi, utafiti wa teknolojia ya matumizi na utafiti wa teknolojia zinazohusika na maslahi ya umma ya jamii. Taasisi ya sayansi ya China na idara za utafiti zinazoendeshwa na vyuo vikuu nyingi zinashughulikia utafiti wa kimsingi. Idara za utafiti za viwanda au makampuni zinashughulikia utafiti wa teknolojia za matumizi. Na Taasisi ya sayansi ya kilimo ya China, Taasisi ya sayansi ya misitu ya China na Taasisi ya sayansi ya hali ya heshima ya China na idara nyingine zinazohusika zinashughulikia utafiti wa kimsingi utakaoleta ufanisi wa jamii.

Taasisi ya sayansi ya China ni idara maarufu na kubwa zaidi kuliko nyingine zote za utafiti wa kisayansi nchini China, ambayo ilianzishwa mwaka 1949, makao makuu yake yako Beijing. Taasisi hiyo ina idara 5 za elimu ya hisabati na fizikia, kemikali, viumbe, jiolojia na teknolojia, pamoja na matawi yake 11 yaliyoko katika sehemu mbalimbali nchini, na ofisi 85 za utafiti, watafiti wake wamefikia elfu 20 ambao wengi wao ni wa kiwango cha juu, na idara zake nyingi ziko katika kiwango cha juu cha utafiti nchini China, baadhi yao zimepewa sifa ya juu duniani.