Utafiti wa ushirikiano kati ya China na nchi za nje
中国国际广播电台

Sayansi haina mpaka, China inapoendeleza sayansi na teknolojia kwa kujitegemea, pia inatilia maanani sana kutumia raslimali za kimataifa ili kuchangia maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China. Hivyo China imefanya shughuli nyingi za maingiliano na ushirikiano wa kimataifa, kushiriki kwenye shughuli nyingi za kimataifa, na kutuma wanasayansi na wanatekenolojia wengi kwenda nchi za nje kusoma na kushiriki katika kazi za utafiti. Wakati huo China inazifungulia mlango nchi za nje katika sekta ya utafiti wa kimsingi na utafiti wa maendeleo ya teknolojia mpya za hali ya juu, kuwakaribisha watu wa nchi za nje kujiunga na kazi ya utafiti wa kisayansi wa China, na kuwatia moyo wanafunzi wa China wanaosoma nchi za nje watoe mchango kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia za China. Hivi sasa idara kadhaa za sayansi na teknolojia za nchi za nje na watu binafsi wameshiriki katika kazi ya utafiti wa kisayansi wa China.

Wakati huo huo wanasayansi na wanateknolojia wa China pia wameshiriki katika mradi mkubwa utafiti wa kisayansi duniani.

Mwaka 2003 China iliwekeana saini mkataba na Umoja wa Ulaya wa kujiunga na Mpango wa Galileo Galilei, pia itashiriki shughuli zote za kutengeneza satlaiti, urushaji na uendelezaji wa bidhaa za matumizi, utungaji wa vigezo na nyinginezo za mpango huo.

China imeshirikiana pia na nchi nyingine husika katika kuanzisha idara za utafiti wa kisayansi kama vile Idara ya utafiti wa teknolojia za software , Kituo cha mawasiliano yenye akili ya China na Hispania, na Kituo cha mawasiliano yenye akili ya China na Uingereza, pamoja na Sehemu ya uanzishaji wa shughuli za sayansi na teknolojia ya Maryland ya China na Marekani, Sehemu ya uanzishaji wa shughuli za sayansi na teknolojia ya China na Uingereza zilizoanzishwa katika nchi za nje.