Maelezo ya jumla

Radio China Kimataifa

Ingawa uendelezaji wa viwanda nchini China umekuwa na historia ya miaka 50 tu, lakini kutokana na nchi kuwa na idadi kubwa ya watu, ongezeko kubwa la uchumi na matatizo kadhaa yaliyosabishwa na sera za zamani, masuala ya mazingira na maliasili yamekuwa makubwa dhahiri nchini China kwa hivi sasa, na hali ya mazingira imekuwa ikikabiliwa na matatizo mengi, kama vile mmomonyoko wa ardhi unazidi kuwa mbaya siku hadi siku, eneo la ardhi inayobadilika kuwa jangwa linapanuka siku hadi siku, eneo la misitu limepungua kwa kiasi kikubwa, mazingira ya kimaumbile yameharibiwa, na aina nyingi za viumbe zimeharibiwa na kupungua hata badhi yao kutoweka, na uchafuzi wa maji na hali ya hewa umekuwa mbaya.

Mwanzoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, chini ya uhimizaji wa mkutano wa mazingira ya binadamu wa Umoja wa Mataifa, kazi ya hifadhi ya mazingira ya China ilianzishwa. Baada ya maendeleo ya zaidi ya miaka 20, China imeanzisha mfumo kamili wa kisheria na kisera wa kushughulikia uchafuzi na kuhifadhi maliasili, na uwekezaji katika hifadhi ya mazingira unaongezeka siku hadi siku. Lakini ikilinganishwa na nchi zilizoendelea, mfumo wa kisera wa hifadhi ya mazingira wa China bado haujakamilika, sera nyingi bado zimewekwa kwenye mipango ya jadi na maagizo ya serikali katika ngazi mbalimbali. Katika sehemu nyingi nchini, idara za serikali za hifadhi ya mazingira bado hazijaongeza nguvu ya utekelezaji wa sheria, na utekelezaji wa sera mbalimbali bado haujaweza kuhakikishwa, hayo yamezuia moja kwa mjoa kuboreshwa kwa hali ya mazingira. Hivi sasa serikali ya China imeongeza zaidi mkakati na sera kuhusu hifadhi ya mazingira, ili kuhakikisha binadamu na mazingira vinaishi kwa kupatana wakati China inapotimiza maendeleo mazuri ya kasi ya uchumi na jamii.