Hali ya mazingira ya maji

Radio China Kimataifa

Maliasili ya maji ya China imekusanyika katika mito 7 mikubwa ya Changjiang, Huanghe, Songhuajiang, Liaohe, Zhujiang, Haihe na Huaihe. "Taarifa kuhusu hali ya mazingira ya China ya mwaka 2003" iliyotolewa na Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China inaonesha kuwa, hali ya uchafuzi kwenye mito 7 mikubwa ya China inazidi kupungua siku hadi siku. Takwimu za mwaka 2003 zimeonesha kuwa, maji ya China yenye sifa ya ngazi ya kwanza, pili na tatu yamechukua 37.7 %, na kiasi hiki cha mwaka 2001 kilikuwa chini ya 33 %.

Katika mifumo 7 ya mito mikubwa, eneo la mtiririko wa Mto Haihe na Mto Liaohe linakumbwa na uchafuzi mbaya zaidi kutokana na takataka za mafuta na uzalishaji wa bidhaa za aina mbalimbali. Ni mito na maziwa pamoja na mabwawa ambayo yamechafuliwa zaidi na madini ya nitrogen na phosphorus, ambapo madini yamezidi kiwango kwenye maziwa na mabwawa.

Sifa ya maji chini ya ardhi kwa ujumla ni nzuri katika miji mingi na sehemu nyingi nchini China, lakini maji hayo ya baadhi ya sehemu pia yamechafuliwa kwa kiasi fulani. Na katika viini vya miji yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na viwanda, maji yaliyoko chini ya ardhi yamechafuliwa vibaya zaidi. Kiasi cha vitu vya kemikali vilivyo ndani ya maji vimekuwa vingi kupita vigezo vilivyowekwa.