Kushughulikia hali ya uchafuzi

Radio China Kimataifa

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China imethibitisha sehemu kadha wa kadha zinazotakiwa kushughulikiwa hali ya uchafuzi, kutunga na kutekeleza mipango ya kushughulikia uchafuzi wa maji kwenye eneo la mtiririko wa mito, sera za usimamizi na sera za udhibiti wa jumla wa utoaji wa maji taka. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, serikali ya China imetenga fedha za renminbi zaidi ya yuan bilioni 40 katika hifadhi ya mazingira ya sehemu ya Bwawa la Magenge Matatu ya Mto Changjiang na eneo la boma. Mwaka 2001, kwenye eneo la Bwawa la Magenge Matatu ya Mto Changjiang, vyanzo vilivyosababisha uchafuzi vilipungua kwa 37, na viwanda 60 vilivyoko kwenye eneo hilo, utoaji wa maji taka ulipungua kwa 15.6 % kuliko mwaka 2000; ujumla wa utaoji wa takataka za aina mbalimbali ulikuwa tani elfu 8. Kuanzia mwaka 2002, eneo la Ziwa Taihu lenye uchafuzi mbaya limeshughulikiwa kwa kazi maalum, ambapo Mto Changjiang unatoa maji yake safi kwa ziwa hilo linalopita eneo la kilomita za mraba 36,900. Kuanzishwa kwa mradi huo kumeboresha dhahiri mazingira ya maji ya eneo la Ziwa Taihu, na kupunguza kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa vitu vya kemikali ndani ya maji, hali hiyo imeboresha kidhahiri hali ya maji ya bomba ya mji wa Shanghai na miji mingine, na watu milioni 10 hivi wamenufaika nayo.

Wakati huo huo, ufuatiliaji na upimaji wa hewa umefanyika kote nchini China. Mwaka 2002, sifa ya hewa katika miji ya kote nchini iliendelea kuboreka, ambapo miji 117 kati ya miji 339 iliyofuatiliwa na idara ya hifadhi ya mazingira, sifa ya hewa ilikuwa nzuri zaidi ya kigezo cha kitaifa cha ngazi ya pili, na sifa ya hewa katika miji 10 kama vile Haikou, Sanya na Zhaoqing ilifika kigezo cha ngazi ya kwanza. Kazi ya kushughulikia hewa ya Beijing imepata ufanisi dhahiri, siku zenye hewa nzuri ambayo sifa yake ilifika kigezo cha ngazi ya pili zilikuwa 201 mwaka 2002, hili ni ongezeko la siku 19 kuliko zile za mwaka 2001. Utoaji wa hewa chafu wa magari katika miji mingi nchini China ulifikia kigezo cha kwanza cha Ulaya, mji wa Beijing na miji mingine mikubwa imeanza kufuata kigezo cha pili cha Ulaya.