Hifadhi ya ardhi oevu

Radio China Kimataifa

angu China ijiunge na "Mkataba wa ardhi oevu wa kimataifa" mwaka 1992, serikali ya China imefanya juhudi za kuokoa na kufufua maliasili za ardhi oevu, ardhi oevu asilia kadha wa kadha zilizowahi kuharibiwa zimehifadhiwa. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, China imejenga sehemu 353 za hifadhi ya ardhi oevu asilia kote nchini zilizopo kando ya bahari, maziwa na mito na ukingoni mwa misitu, na sehemu 21 miongoni mwao zimeorodheshwa kwenye arodha ya ardhi oevu muhimu duniani, eneo la sehemu hizo limefika hekta milioni 3.03.

"Mpango wa utekelezaji wa hifadhi ya ardhi oevu ya China" unaotekelezwa kuanzia mwezi Novemba mwaka 2000 ulitungwa na wizara 17 za baraza la serikali la China ikiwemo wizara ya misitu ya China. Kutokana na mpango huo, ifikapo mwaka 2010, China itadhibiti mwelekeo wa kudidimia kwa ardhi oevu kutokana na shughuli za binadamu, na ifikapo mwaka 2020, ardhi iliyodidimia au kupotezwa itafufuliwa siku hadi siku.