Hifadhi ya aina nyingi za viumbe

Radio China Kimataifa

China ikiwa moja kati ya nchi zilizotangulia kusaini "Mkataba wa aina nyingi za viumbe", siku zote inashiriki kwa juhudi katika mambo ya kimataifa yanayohusu mkataba huo, na kutoa maoni kuhusu masuala makubwa ya utekelezaji wa mkataba huo. China vilevile ni moja kati ya nchi chache zilizotangulia kukamilisha mpango wa utekelezaji wa mkataba huo. "Mpango wa China wa utekelezaji wa hifadhi ya aina nyingi za viumbe" uliokamilika mwaka 1994, umezifanya shughuli nyingi za hifadhi ya mazingira ya viumbe ziweze kufanyika kwa kufuata kanuni zilizowekwa kwenye mkataba huo. Kutokana na "Sheria ya hifadhi ya wanyama pori", kitendo chochote cha kuharibu maliasili ya wanyama pori kitaadhibiwa, na mtu atakayefanya uhalifu huo anaweza kuhukumiwa kifo.

Idara husika za serikali zinazingatia sana hifadhi yenye ufanisi ya maliasili za viumbe. Mwezi Januari mwaka 2003, Taasisi ya sayasni ya China ilitetea kuanzisha mradi wa kuokoa mimea inayokabiliwa na hatari ya kutoweka, inapanga kuongeza aina elfu 13 za mimea inayohifadhiwa kwenye bustani 12 za mimea kuwa aina elfu 21, na kujenga bustani kubwa kabisa la mimea duniani lenye eneo la kilomita za mraba 458. Katika mradi huo, fedha za renminbi zaidi ya yuan milioni 300 zitatumika katika kukusanya mimea adimu inayokaribia kutoweka, na kujenga ghala ya gene za mimea katika sehemu muhimu za Milima Qinglin, mji wa Wuhan, Xishuangbanna na Beijing.

Mafanikio ya hatua ya mwanzo yamepatikana katika mradi wa kuokoa wanyama pori wanaokaribia kutoweka, hivi sasa vituo 250 vya kuzaliana kwa wanyama pori vimejengwa nchini kote China, ambapo unatekelezwa mradi maalum wa kuokoa aina 7 za wanyama pori kama vile panda wakubwa na ndege kwarara. Hivi sasa panda wakubwa ambao wamechukuliwa kuwa ni "hazina ya taifa" na kusifiwa kuwa ni "visukuku hai" wamehifadhiwa na kudumishwa kuwa zaidi ya 1000, na mazingira yao ya kuishi yanaendelea kuboreshwa; kundi la ndege ina ya Kwarara mwenye kishungi (crested ibis) limeongezeka kuwa ndege 250 kutoka 7, hali ya kukaribia kutoweka inapungua zaidi; idadi ya mamba wa Yanzi inakaribia elfu 10; (eld’s deer) paa wa Hainan imeongezeka na kuwa zaidi ya 700 kutoka 26; kundi la ndege aina ya shakwe wa zamani (relicgull) limeongezeka na kuwa zaidi ya elfu 10 kutoka 2000; chui walioonekana nadra wamejitokeza mara kwa mara katika sehemu ya kaskazini mashariki, mashariki na kusini ya China; kazi ya utafiti kuhusu hali ya kuzaana kwa pomboo wenye mapezi meupe pia inafanyika kwa haraka; Kutokana na kazi isiyolegea ya kupiga vita uwindaji wa haramu, pamoja na kushirikiana na jumuiya kadhaa za kimataifa za hifadhi ya wanyama, swala wa Tibet waliouawa kiharamu na kupungua kwa haraka wamepata nafasi ya kuzaliana katika hali ya utulivu, hivi sasa idadi ya swala wa Tibet imedumishwa kuwa elfu 70 hivi.