Ujenzi wa sehemu ya hifadhi ya maumbile

Radio China Kimataifa

Hifadhi ya maumbile ya kwanza ya China ilianzishwa kwenye sehemu ya Mlima Dinghu ya Chaoqing mkoani Guangdong mwaka 1956. Hifadhi ya maumbile ya chanzo cha mito mitatu iliyoanzishwa mwezi Agosti mwaka 2000 ni sehemu kubwa kabisa yenye mwinuko wa juu kabisa kutoka uso wa bahari ambayo ni hifadhi ya maumbile yenye viumbe wengi kabisa. Hifadhi hiyo iko kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, ambayo iko katika sehemu ya chanzo cha Mto Changjiang, Mto Manjano na Mto Lancangjiang. Ilipofika mwishoni mwa mwaka 2002, sehemu za aina mbalimbali za hifadhi ya maumbile zipatazo 1757 zilijengwa kote nchini China, eneo la jumla la hifadhi hizo limefikia hekta milioni 132.95, ambalo ni 13.2 % ya eneo la jumla la nchi kavu ya China. Sehemu hizo za hifadhi ya maumbile zimefanya kazi muhimu za kutunza vyanzo vya mito, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, kuzuia upepo na kuimarisha mchanga na kuboresha hali ya hewa ya kikanda; na sehemu nyingi za hifadhi ya maumbile zimekuwa sehemu muhimu ya hifadhi ya aina nyingi za viumbe duniani. Na mkoani Yunnan kuna sehemu nyingi zaidi za hifadhi ya maumbile kuliko mikoa mingine, sehemu hizo zimefikia 152 na eneo la sehemu hizo zimefikia hekta milioni 2.8. Sehemu 22 kama vile hifadhi ya maumbile za Wolong na Jiuzaigou mkoani Sichuan, Mlima Changbei mkoani Jilin, Mlima Dinshan mkoani Guangdong na Mto Beishui mkoani Gansu zimeorodheshwa na shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa kuwa “sehemu za hifadhi ya viumbe duniani”.