Maendeleo ya hifadhi ya mazingira ya China

Radio China Kimataifa

Maendeleo ya kazi ya hifadhi ya mazingira ya China

Baada ya kufanya juhudi za zaidi ya miaka 30 iliyopita, mafanikio yaliyotambuliwa duniani yamepatikana katika hifadhi ya mazingira ya China. Katika mchakato wa kurekebisha miundo ya kiuchumi na kuongeza mahitaji nchini, China imeongeza kidhahiri nguvu ya hifadhi ya mazingira. Kwa ujumla, imedhibiti mwelekeo wa uchafuzi unaozidi kuwa mbaya kote nchini, na hali ya mazingira ya miji na sehemu kadhaa imeboreshwa kwa kiasi fulani na kuchangia utekelezaji wa mikakati ya maendeleo endelevu nchini China.

Serika yazingatia kazi ya hfiadhi ya mazingira

Kuanzia mwaka 1997, serikali ya China inafanya kongamano kila mwaka ili kusikiliza ripoti kuhusu kazi ya hifadhi ya mazingira na kufanya mpango wa kazi hiyo. Viongozi wa China wanaona kuwa hifadhi ya mazingira ni mambo makubwa ya kusitawisha nchi na kuleta heri na baraka kwa wananchi, kazi hiyo inahusiana na usalama wa mazingira ya taifa. Kuhifadhi mazingira ni kulinda nguvu kazi. Kumekuwa na ulazima wa kujenga na kukamilisha utaratibu wa utoaji sera na hatua kuhusu mazingira na maendeleo, maofisa wa serikali za mikoa mbalimbali wanatakiwa kuongoza wenyewe utekelezaji wa jukumu hilo. Lazima kuimarisha usimamizi wa pamoja wa hifadhi ya mazingira, kutenga fedha zaidi katika hifadhi ya mazingira na kuhamasisha watu kushiriki katika kazi hiyo. Ni lazima kushikilia kuifanya kazi ya kuzuia na kushughulikia hali ya uchafuzi iende sambamba na hifadhi ya hali ya viumbe. Na lazima kuweka mkazo katika kazi muhimu, na kuweka mkazo katika kuzuia na kushughulikia hali ya uchafuzi katika miji, eneo la mtiririko wa maji, kanda au eneo la bahari.

Katika mageuzi ya idara za serikali, idara za hifadhi ya mazingira zimeimarishwa siku hadi siku. Mwaka 1988, idara ya taifa ya hifadhi ya mazingira ilikuwa idara inayotawaliwa moja kwa moja na Baraza la serikali. Mwaka 1993, idara hiyo ilikuwa idara ya ngazi ya wizara ndogo chini ya Baraza la serikali. Mwaka 1998, idara hiyo imekuwa idara kuu ya taifa ya hifadhi ya mazingira.

Uchafuzi wa mazingira wadhibitiwa

Katika miaka kadhaa ya hivi karibuni, China ilifunga na kupiga marufuku mashirika madogo zaidi ya elfu 84 yaliyoleta uchafuzi mbaya, ambapo zaidi ya 90 % ya viwanda vilivyotoa uchafuzi vilitimiza lengo la kufikia kigezo cha utoaji uchafuzi.

Mafanikio yamepatikana katika kipindi cha kushughulikia kazi ya kupunguza uchafuzi katika sehemu zenye hali mbaya ya uchafuzi. Hali ya uchafuzi ya eneo kubwa la Mto Huai ilipungua kidhahiri, hali ya uchafuzi ya Mto Hai na Mto Liao ilipungua kwa kiasi fulani, na hali ya maji ya Ziwa Taihu iliyozidi kuwa mbaya ilidhibitiwa kwa hatua ya mwanzo, na hali ya kuzidi kwa madini ya nitrogen na phosphorus ilipungua kwa kiasi fulani, hali mbaya ya Ziwa Chao kuwa madini mengi ya nitrogen na phosphorus ilidhibitiwa kimsingi. Na mafanikio makubwa yamepatikana katika kazi ya kushughulikia hali mbaya ya uchafuzi wa hewa. Na kazi ya kukinga na kushughulikia hali ya uchafuzi wa bahari ya Bo imeanzishwa kwa pande zote.

Hifadhi na ujenzi wa mazingira ya viumbe vyaimarishwa

China imetekeleza sera ya kuzifanya kazi za kinga na udhibiti wa hali ya uchafuzi na hifadhi ya mazingira ya viumbe ziende sambamba na kutiliwa maanani sawasawa, pia imeharakisha hifadhi na ujenzi wa mazingira ya viumbe. Kwa ujumla sehemu 1227 za aina mbalimbali za hifadhi ya maumbile ya kiasili zimejengwa kote nchini, eneo la sehemu hizo limekuwa na hekta milioni 98.21, eneo hilo ni 9.85 % la ardhi ya China. Serikali kuu imeidhinisha mipango ya majaribio ya kujenga mikoa minne ya mazingira ya viumbe, na sehemu za ngazi ya kitaifa zaidi ya 200 ya vielelezo vya mazingira ya viumbe.

Serikali kuu imetekeleza hatua ya kufunga milima na kutunza misitu katika sehemu kubwa za misitu nchini, eneo la sehemu hizo limefikia hekta milioni 5.186. Na mikoa, mikoa inayojiendesha na miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu ipatayo 13 imesimamisha shughuli za kukata miti katika misitu asilia. Eneo la misitu kote nchini China limefikia 16.5 %.

Maendeleo yapatikana katika ujenzi wa utaratibu wa kisheria

Hivi sasa China imerekebisha "sheria ya kinga na udhibiti wa uchafuzi wa hewa", "sheria ya kinga na udhibiti wa uchafuzi wa maji" na "sheria ya hifadhi ya mazingira ya bahari"; na kutunga "sheria ya kinga na udhibiti wa uchafuzi wa makelele kwa mazingira", "kanuni halisi za utekelezaji wa sheria ya kinga na udhibiti wa uchafuzi wa maji", "vifungu vya hifadhi ya mazingira katika miradi ya ujenzi" na kadhalika. Mpaka sasa China imetangaza sheria 6 kuhusu hifadhi ya mazingira, sheria 10 kuhusu maliasili husika na sheria zaidi ya 30 kuhusu hifadhi ya mazingira, kutoa kanuni zaidi ya 90 kuhusu hifadhi ya mazingira, kuthibitisha vigezo 430 vya kitaifa kuhusu hifadhi ya mazingira, na sheria 1,020 za kisehemu kuhusu hifadhi ya mazingira.

Kutenga fedha zaidi katika hifadhi ya mazingira

Tokea mwaka 1996 hadi mwishoni mwa mwaka 2000, China ilitenga fedha yuan bilioni 360, hili ni ongezeko la yuan bilioni 230 kuliko zile za muda wa kuanzia mwaka 1990 hadi 1995, ambazo zilifikia 0.93 % ya pato la taifa. Hasa katika miaka kadhaa ya hivi karibuni, serikali kuu ya China ilitoa dhamana ya kitaifa ya muda mrefu, fedha za yuan bilioni 46 miongoni mwao zimetumika katika kinga na udhibiti wa hali ya uchafuzi na ujenzi wa mazingira ya viumbe, ambazo zimechangia kazi ya kuboresha sifa ya mazingira, kuongeza matumizi nchini na kuhimiza ongezeko la uchumi.

Mwamko wa wananchi kuhusu hifadhi ya mazingira waongezeka

Hivi sasa watu wa jamii nzima ya China wamekuwa na uchangamfu zaidi katika kufuatilia, kuunga mkono na kushiriki katika shughuli za hifadhi ya mazingira. Kuanzia mwaka 1998 hadi 1999, Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa na Wizara ya elimu ya China zilikabidhi Kituo cha utafiti wa hali ya nchi katika Chuo kikuu cha Beijing kazi ya kufanya uchunguzi na kuwahoji wakazi wa familia karibu elfu 10 kwenye wilaya 139, matokeo ya uchunguzi huo yameonesha kuwa, suala la mazingira limekuwa suala linalofuatiliwa zaidi na watu katika jamii. Elimu kuhusu hifadhi ya mazingira imewekwa kwenye elimu ya lazima ya miaka 9. Na shughuli za kujenga shule na sehemu za mitaa kuwa sehemu zisizo na uchafuzi zinaleta athari kubwa zaidi na zaidi kwa jamii.

Serikali ya China inawahamasisha wananchi washiriki kwenye shughuli za hifadhi ya mazingira. Na imeanzisha simu ya No.12369 inayopokea taarifa kuhusu vitendo vya uharibifu wa mazingira. Serikali imeongeza nguvu ya upashanaji habari kuhusu hali ya mazingira, kila siku inatoa habari kuhusu sifa ya hewa ya miji muhimu 47, kila wiki inatoa habari kuhusu sifa ya maji kwenye maeneo muhimu ya mito, na kila wiki inatoa habari kuhusu hali ya maji kwenye viwanja vikubwa vya kuogelea baharini. Na kabla na baada ya siku ya mazingira ya dunia ya tarehe 5 Juni ya kila mwaka, serikali hutoa habari kuhusu hali ya sifa ya mazingira ya nchi nzima katika mwaka uliotangulia.