Malengo ya hifadhi ya mazingira ya China

Radio China Kimataifa

Maelengo ya hifadhi ya mazingira yaliyothibitishwa na China ni kama yafuatayo: Hali ya uchafuzi wa mazingira ipungue kwa kiasi fulani mwaka 2005, hali ya uchafuzi wa mazingira inayozidi kuwa mbaya idhibitiwe kwa hatua ya mwazo, hali ya sifa ya mazingira ya miji na vijiji hasa miji mikubwa na ya wastani na sehemu muhimu iboreshwe, na sheria, sera na mfumo wa usimamizi wa hifadhi ya mazingira zinazoweza kulingana na mfumo wa uchumi wa soko huria wa ujamaa vikamilishwe.

Mwaka 2005, utoaji wa madini, moshi na mavumbi na takataka zinazoleta uchafuzi kutoka viwandani ulipungua kwa 10% kuliko mwaka 2000.

Ili kutimiza lengo la hifadhi ya mazingira ya mpango wa 10 wa miaka mitano ya uchumi na jamii wa China, gharama za hifadhi ya mazingira ya nchi nzima ya China zinatakiwa kufikia Yuan bilioni 700 ambayo ni 1.3% ya thamani ya jumla ya uzalishaji wa nchini wa kipindi hicho.