Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa

Radio China Kimataifa

Mwaka 1998, kutokana na uthibitishaji wa mkutano wa kwanza wa Bunge la 9 la umma la China na mpango husika wa Baraza la serikali la China kuhusu mageuzi ya mashirika, China iliweka rasmi Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa (ngazi yake inalingana na wizara). Jukumu lake kuu ni kutunga sera na sheria za hifadhi ya mazingira ya nchi, kutunga kanuni za utawala, kusimamia shughuli za uendelezaji na matumizi ya maliasili katika sehemu za maumbile zinazoweza kuleta athari mbaya kwa hifadhi ya mazingira ya viumbe, ujenzi wa miradi muhimu ya mazingira ya viumbe na kazi ya kufufua hali ya uharibifu kwa mazingira ya viumbe na kadhalika. Idara hiyo kuu pia ina idara zake kwenye ngazi mbalimbali. Na mkuu wa hivi sasa wa Idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa ya China ni Bwana Xie Zhenhua.

Anuani ya tovuti ya idara hiyo ni: http://www.zhb.gov.cn