Kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China

Radio China Kimataifa

Mwaka 1992, serikali ya China iliidhinisha Kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China. Kamati hiyo ni idara ya utoaji ushauri ya kimataifa ya ngazi ya juu, wadhifa wa mwenyekiti wake huchukuliwa na mawaziri au manaibu mawaziri wa baraza la serikali la Jamhuri ya watu wa China (mwenyekiti wake wa sasa ni naibu waziri mkuu Bwana Zeng Peiyan). Jukumu lake kuu ni kutoa mapendekezo ya kisera kuhusu masuala makubwa, muhimu na ya dharura yanayohusu sekta za mazingira na maendeleo ya China, pia kutoa vielelezo vya kisera na kimradi. Kamati hiyo inaundwa na mawaziri au manaibu mawaziri, wataalamu mashuhuri wa sekta ya mazingira na maendeleo, maprofesa pamoja na mawaziri wa nchi nyingine na viongozi wa jumuia za kimataifa.

Anuani ya tovuti ya kamati hiyo kwenye mtandao wa Iternet ni: http://www.cciced.org