Mfuko wa hifadhi ya mazingira ya China 

Radio China Kimataifa

Mfuko huo ulianzishwa mwezi Aprili mwaka 1993, ambao ni shirikisho la jamii lisilotafuta faida na lenye haki ya kuwa mwakilishi wa kisheria, nao ni mfuko wa kwanza wa kiraia wa China unaoshughulikia shughuli za hifadhi ya mazingira. Mfuko huo unafuata kanuni ya "kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi, kuzitumia fedha hizo kwa kuwahudumia wananchi na kuleta heri na baraka kwa binadamu", ukichangisha fedha kwa njia mbalimbali, na kuzitumia kwa kuwatunukia mashirika au watu waliotoa mchango mkubwa kwa kuhifadhi mazingira ya China, kusaidia shughuli na miradi ya aina mbalimbali inayohusika na hifadhi ya mazingira, kuanzisha maingiliano na ushirikiano wa kiteknolojia na nchi za nje katika sekta ya hifadhi ya mazingira, kusukuma mbele maendeleo ya kazi mbalimbali za hifadhi ya mazingira kama vile usimamizi wa hifadhi ya mazingira ya China, utafiti wake wa kisayansi, uenezi na utoaji elimu, kuwaandaa wataalamu wa hifadhi ya mazingira, kufanya maingiliano ya kitaaluma, kuendeleza shughuli za hifadhi ya mazingira na shughuli mbalimbali zinazohusiana na nchi za nje.

Anuani ya tuvuti ya Mfuko wa hifadhi ya mazingira ya China (CEPF) kwenye mtandao wa internet ni : http://www.cepf.org.cn/