Shirikisho la Marafiki wa dunia ya maumbile

Radio China Kimataifa

Tawi la utamaduni wa dunia ya maumbile la Chuo cha utamaduni wa China (kwa kawaida linaitwa "Shirikisho la marafiki wa dunia ya maumbile") ni kundi la kwanza la kiraia la hifadhi ya mazingira lililoidhinishwa na serikali ya China mwezi Machi mwaka 1994. Mwazilishi wake na mkuu wake wa sasa ni Profesa Liang Congjie. Shirikisho hilo linafuata nia ya kuanzisha elimu ya kiumma ya hifadhi ya mazingira, kutetea ustaarabu wa hifadhi ya mazingira ya kimaumbile, kutetea na kueneza utamaduni wenye umaalumu wa kichina kuhusu hifadhi ya mazingira na kusukuma mbele maendeleo ya hifadhi ya maumbile ya China.

Tovuti ya shirikisho hilo kwenye mtandao wa internet ni: http://www.fon.org.cn/