Ushirikiano na maingiliano ya kimataifa kwenye sekta ya mazingira

Radio China Kimataifa
 

China ikiwa nchi kubwa kabisa inayoendelea na nchi yenye mazingira makubwa zaidi, imekuwa mhusika kwenye sekta ya mazingira ya kimataifa. China inafanya juhudi kubwa katika kushiriki shughuli za kidiplomasia kuhusu mambo ya mazingira duniani, na imetoa mchango na kufanya kazi za kiujenzi katika sekta za mazingira na maendeleo duniani

Mwaka 1972, ujumbe wa serikali ya China ulihudhuria mkutano wa kwanza kuhusu mazingira ya binadamu uliofanyika huko Stockholm. Mwaka 1992, waziri mkuu wa wakati huo Li Peng aliongoza ujumbe wa serikali ya China kuhudhuria mkutano wa wakuu kuhusu mazingira na maendeleo uliofanyika huko Rio de Janeiro, ambapo China ilitangulia kusaini "Mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa" na "Mkataba kuhusu aina nyingi za viumbe", hatua hiyo imesifiwa sana na jumuia ya kimataifa. Mwezi Agosti mwaka 2002, waziri mkuu Zhu Ronji aliongoza ujumbe wa serikali ya China kuhudhuria mkutano wa wakuu kuhusu maendeleo endelevu uliofanyika huko Johannesburg, ambapo alitangaza kuwa serikali ya China imethibitisha na kukubali "Mkataba wa Kyoto", hatua hii ilisifiwa na watu wengi wa jumuiya ya kimataifa.

Katika mkutano wa mazingira ya kimataifa na mazungumzo ya mkataba wa kimataifa, China ilishikilia tangu mwanzo hadi mwisho kanuni kuhusu nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea zinabeba wajibu wa pamoja ambao pia wa tofauti katika kulinda mazingira ya dunia nzima, ambapo China inasimama imara kwenye upande wa nchi zinazoendelea, inapinga umwamba kwenye sekta ya mazingira, na kupinga kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa kisingizio cha suala la mazingira. Kutokana na historia na hali halisi ya hivi sasa, nchi zilizoendelea zote ni nchi zinazobeba wajibu mkubwa kuhusu suala la mazingira, na nchi zinazoendelea ni nchi zinazodhuriwa. Hivyo nchi zilizoendelea zinabeba jukumu la kuchukua hatua kwanza na kuzisaidia nchi zinazoendelea katika juhudi zao za kushiriki kwenye shughuli za kulinda mazingira ya dunia nzima.

Aidha, jumuiya za kiraia za hifadhi ya mazingira za nchi mbalimbali duniani kama vile Mfuko wa mazingira asilia ya dunia, na Mfuko wa kulinda wanyama duniani zimeanzisha ushirikiano na idara husika na jumuiya za kiraia za China, na matokeo yenye juhudi yamepatikana katika shughuli hizo.

China imevumbua kwanza aina ya "kamati ya ushirikiano wa kimataifa wa mazingira na maendeleo ya China". Kamati hiyo iliundwa na watu mashuhuri na wataalamu duniani zaidi ya 40, ambayo ni shirika la ngazi ya juu la utoaji ushauri la serikali. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, kamati hiyo imetoa mashauri mengi ya kiujenzi kwa serikali ya China, kamati hiyo imesifiwa kuwa ni mfano wa kuigwa wa ushirikiano wa mazingira ya kimataifa.