China na “Mkataba wa aina nyingi za viumbe”

Radio China Kimataifa
 

Baada ya kufanyika kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira na maendeleo mwaka 1992, serikali ya China imezingatia hali yake halisi ya nchi, ikiwa na msimamo wa makini inatekeleza ahadi yake kwenye mkutano huo, kuthibitisha mikakti ya maendeleo endelevu ya uchumi wa taifa, na kuonesha ipasavyo mawazo ya mikakati hiyo katika sera mbalimbali za uchumi wa nchi. Mwaka 1994, Baraza la serikali la China liliidhinisha na kutangaza “Waraka kuhusu idadi ya watu, mazingira na maendeleo ya China katika karne ya 21”, waraka huo umeonesha vilivyo mikakati ya maendeleo endelevu ya nchi. Mwaka 1996 Bunge la umma la China lilipitisha “Mpango wa 9 wa miaka mitano kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii ya Jamhuri ya Watu wa China na Mwongozo wa malengo ya mbali ya mwaka 2010”, hii imebainisha zaidi sera ya China ya kushikilia mikakati ya maendeleo endelevu.

Serikali ya China inaona kuwa, matumizi ya kudumu ya maliasili na mazingira mazuri ya viumbe ni masharti ya kwanza katika kutekeleza mikakati ya maendeleo endelevu. China imechukua hatua za kulinda aina nyingi za viumbe, kuzuia mmomonyoko wa ardhi na hali ya jangwa kwenye ardhi, kuendeleza eneo la misitu na kuboresha mazingira ya viumbe mijini na vijijini, kukinga na kudhibiti uharibifu na uchafuzi kwa mazingira, na kushiriki kwa juhudi ushirikiano wa dunia nzima katika hifadhi ya mazingira, ili kutekeleza kwa ufanisi mikakati ya maendeleo endelevu. Mambo kuhusu kulinda aina nyingi za viumbe ili kuzitumia mwaka baada ya mwaka yameoneshwa katika sera, mipango na kazi mbalimbali za idara zote za serikali na mipango ya maendeleo ya uchumi na jamii ya serikali za mitaa za ngazi mbalimbali.

Katika mchakato wa mpito wa kuanzishwa kwa uchumi wa soko huria badala ya uchumi wa mipango wa jadi, serikali ya China imefanya juhudi katika kuhimiza uzalishaji wa kilimo wa njia ya kisayansi na kiteknolojia ili kupata ongezeko la uchumi. Kutokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu na matumizi ya maliasili kupita kiasi, hali ya mazingira ya viumbe inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, hali ya mmomonyoko wa ardhi, na hali ya ardhi inayobadilika kuwa jangwa inazidi kuwa mbaya, na maliasili za viumbe zinatumika kwa haraka kupita kiasi, yote hayo yamekwamisha vibaya maendeleo ya uchumi wa taifa, hasa kuzidisha hali ya umaskini kwenye sehemu zenye uharibifu wa mazingira ya viumbe. Serikali ya China inazingatia mageuzi ya sera za uchumi wa vijijini, kuwahamasisha wakulima kutumia njia ya kisayansi na kiteknolojia katika uzalishaji wa mazao, kuanzisha miradi ya ujenzi wa mazingira ya viumbe kama vile kupanda miti na majani na kuendeleza misitu, kushughulikia hali ya mmomonyoko wa ardhi na kuondoa hali ya jangwa, kuendeleza teknolojia ya kilimo cha kiviumbe na kadhalika. Hatua hizo zitatekelezwa na kwenda sambamba na kuendeleza uzalishaji mazao ya kilimo na kulinda aina nyingi za viumbe ili kudumisha matumizi ya kudumu.

Katika miaka mingi iliyopita, China imepata uzoefu mwingi wenye manufaa katika ujenzi wa mazingira ya viumbe kote nchini, kama vile uzoefu wa kujenga misitu mikubwa ya kukinga upepo, na kujenga mazingira yenye majani kwenye jangwa; kutengeneza mashamba kwenye miteremko ya milima kuwa mashamba ya kulima na kujenga mashamba yanayoweza kuzalisha mazao mengi zaidi katika hali ya utulivu; kujenga mejengo makubwa ya kuhifadhi maji mashambani na kufanya ujenzi wa miradi midogo ya kulimbikiza maji na kuzuia mmomonyoko wa ardhi; kurudisha misitu na malisho kwenye ardhi iliyotumiwa kwa kilimo, na kufufua hali ya mazingira ya maumbile ya kiasili; kupanda miti ya kiuchumi, kujenga misitu asilia na kupanda miti na majani kwa pamoja; kuanzisha shughuli za kilimo kwa kubana matumizi ya maji, na kutumia teknolojia za kisasa; kujenga mazingira yenye milima, maji, mashamba, misitu na barabara, na kuboresha hali ya eneo dogo la mitiririko ya mito; kupanda miti na majani kwenye milima iliyoachwa; kushughulikia hali ya kuvia, kuwa ya jangwa na kuwa na madini ya alkali kwa malisho na kadhalika, uzoefu huo na hatua za utekelezaji zote zimefanya kazi muhimu zenye juhudi kwa kulinda aina nyingi za viumbe.