Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2004-08-10 20:58:13    
Mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Miaka 55 ya China mpya"

cri
   Wasikilizaji wapendwa:

    Tarehe mosi Oktoba mwaka huu Jamhuri ya watu wa China itatimiza miaka 55 tangu kuzaliwa kwake. Ili kuadhimisha siku hiyo, kuanzia tarehe 15 Agosti mwaka huu Radio China kimataifa itaanzisha mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa "Miaka 55 ya China mpya", mashindano hayo yataendelea mpaka mwishoni mwa mwezi Novemba.

    Katika chemsha bongo ya ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya, tutatangaza makala 4 kwenye matangazo yetu ya radio na kwenye tovuti yetu. Makala hizo nne zitafahamisha maendeleo ya uchumi wa China, mambo ya kidiplomasia ya China, hali ilivyo sasa ya elimu ya China na hali kuhusu mikoa inayoendesha ya makabila madogomadogo na maendeleo ya makabila mbalimbali. Kama ilivyokuwa kwa mashindano ya chemsha bongo yaliyopita, kila tukisoma makala moja tutatoa maswali mawili, ambayo wasikilizaji wetu mtatakiwa kuyajibu.

    Kamati ya uchaguzi wa wasikilizaji washindi, itachagua wasikilizaji watakaopata nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu. Watakaopata nafasi ya kwanza, watashiriki katika uchaguzi wa washindi wa nafasi maalum. Wasikilizaji watakaopata nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu watapewa zawadi nzuri, na washindi wa nafasi maalum wataalikwa kuja kuitembelea China kwa wiki moja.

    Tunawakaribisha wasikilizaji wetu mshiriki katika mashindano hayo ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa miaka 55 ya China mpya, na tunawatakia mafanikio mema.

    Tunapenda kuwaarifu kuwa, barua kuhusu mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Miaka 55 ya China mpya pamoja na masuali manane ya makala 4 kwa ujumla tutamtumia kila msikilizaji hivi karibuni. Makala ya kwanza itasomewa tarehe 15 Agosti, kwenye kipindi cha sanduku la barua. Karibuni.

    Kuna jambo moja ambalo tunapenda kuwaarifu wasikilizaji wetu. Hivi karibuni tumekuwa tukipkeaa barua mara kwa mara kutoka kwa wasikilzaji wetu ambao wanalalamika kuwa wametuletea kadi nyingi za salamu lakini hawazisikii zikisomwa katika kipindi cha salamu zenu. Kwa kweli hapa inatubidi tuwaombe radhi kwa wasikilizaji wetu, na kuwaomba watuelewe kuwa muda wa kipindi cha salamu zenu una kikomo. Kila siku tuna dakika 3 na sekonde 8 au 9 hivi. Ingawa tunajitahidi kusoma kila kadi, lakini kadi bado ni nyingi hata hivyo tunajitahidi kuendelea kuzisoma. Na kama tukikubaliwa siku za usoni tutaweza kuongeza muda wa kipindi hiki.

    Kuanzia katikati ya mwezi huu, idara yetu itaongezewa nguvu mpya, kwani baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya lugha ya Kiswahili wamechaguliwa kujiunga na idhaa yetu. Tukipanga vizuri, baada ya kusoma kadi zenu za salamu, pia tutaziweka kwenye tovuti yetu, ili salamu hizo zipeperushwe hewani na kwenye mtandao wa internet.

    Tunawakarisha wasikilizaji wetu watuandikie barua au kutuletea barua pepe kutoa maoni na mapendekezo yenu kuhusu vipindi vyetu kwenye matangazo na kwenye tovuti yetu ili tuweze kuboresha zaidi vipindi vyetu na kuwahudumia vizuri zaidi wasikilizaji wetu.  Msisahau anuani ya tovuti yetu kwenye mtandao wa internet yaani www.cri.cn .Karibuni

Idhaa ya Kiswahilil 2004-08-10