Kuna msemo maarufu usemao: "Rafiki mpime kwa vitendo". Ama kwa kweli usemi huu unatumika mara nyingi kutilia mkazo vitendo vya watu walio kwenye mahusiano ya karibu. Hakika, ni rahisi kwa mtu binafsi kupima umuhimu wake anapoangalia mambo anayotendewa.
Msemo huu ni muhimu hasa wakati ambapo, kote duniani, mataifa yanatazamia kujenga urafiki wa kweli na wa kudumu. Inatarajiwa kwamba urafiki wa aina hiii utazaa manufaa kwa pande zinazohusika.
Kila mkereketwa wa matukio ya kimataifa bila shaka kwa sasa anafuatia kwa karibu hatua zozote zinazochukulia na China, ambayo bila shaka, ni taifa lenye uchumi unaoongezeka kwa kasi duniani. Hii imekuwa ndio hali halisi hasa baada ya kiongozi wake wa sasa kuendeleza sera za ujenzi wa jamii yenye manufaa kwa wote.
Afrika kwa sasa imeonekana kufurahia China inavyoendesha shughuli zake. Isitoshe, mataifa 50 za Afrika vimesajili uhusiano wa kidiplomasia na nchi hiyo inayotawalia na Chama cha Kikomunisti.
Ziara ya kwanza ya mwaka nje ya nchi
Jambo la kuvutia, ni utamaduni unaoendelezwa na China ambapo mawaziri wake wa kigeni daima wamechagua Afrika kama sehemu wanaosafiri kwanza nje ya nchi katika Mwaka Mpya kabla ya kuzuri nchi nyingine. Desturi hii imekithiri kwa kwa miaka 20 iliyopita. Hata hivyo mwaka 2018 haina tofauti. Waziri Wang Yi ameanza ziara ya nchi tano za Afrika ambako atafanya ziara rasmi kwenye mataifa ya Rwanda, Angola, Gabon, na Sao Tome na Principe kuanzia Januari 12 hadi Januari 16.
"Juhudi za Waziri Wang Yi za kuendeleza utamaduni huu unaonyesha dhahiri kwamba China mara kwa mara inatilia mkazo mahusiano baina ya China na Afrika" Alisema msemaji wa katika wizara ya mambo ya nje bwana Lu Kang hivi karibuni kwa vyombo vya habari katika mkutano mjini Beijing.
Ama kwa hakika, ziara hii hasa inalenga kuimarisha urafiki ambao tayari upo kati ya China na Afrika. Kwa kweli, urafiki huu haupo tena katika utupu. Umekitwa katika majukwaa halisi na dhabiti ambayo kwa sasa ni mikakati mwafaka. Jukwaa la ushirikiano wa China na Africa (FOCAC) ni mojawapo wa jukwaa hizi.
"Ziara ya Wang itakuza Imani ya kisiasa, kuimarisha ufanisi wa pamoja, na kusaidia maandalizi kwa ajili ya mkutano ujao wa jukwaa la ushirikiano katika ya China na Afrika (FOCAC), ambayo China itakuwa mwenyeji mwaka huu". Lu alisema.
Vikwazo vya maendeleo Afrika
Katika mkutano wa FOCAC uliofanyika mwaka wa 2015 nchini Afrika Kusini, rais Xi Jinping alitangaza maeneo 10 kubwa ya ushirikiano. Mpango huo unaogharimu bilioni 60 dola za Marekani ulitambuliwa kama njia moja ya kusisimua sekta muhimu ya uchumi kama vile viwanda, kilimo cha kisasa, miundombinu, huduma za kifedha, uwezeshaji wa biashara na uwekezaji, kupunguza umaskini na ustawi wa umma, afya ya umma, kuimarisha mahusiano kati ya watu wa taifa moja hadi nyingine, na amani na usalama.
"Sisi tutangatia usaidizi wetu kwa nchi za Afrika hasa katika kumaliza vikwazo vya maendeleo tatu ambayo ni yale ya miundombinu mbovu, uhaba wa vipaji, na uhaba wa fedha." Rais Xi alisisitiza
Katika hotuba yake kwa marais wa nchi mbalimbali ya Afrika na viongozi wa serikali wakati huo, kiongozi huyo wa China alitoa hakikisho kuwa nchi yake ina nia moja tu ya kusaidia mataifa yenye uchumi dhaifu barani humo kuafikia maendeleo huru na endelevu.
Lakini kwa kuwekeza asilimia kubwa ya rasilimali za kifedha kwa mpango huu, China ilikuwa tayari inaonyesha nia yake ya kutekeleza maendeleo ya bara la Afrika. Mipango yote 10 yaliyotangazwa wakati huo kwa sasa yamo katika hatua ya utekelezaji. Bila shaka, miradi mikubwa ya viwanda na miundombinu yaliyoanzishwa na serikali ya China moja kwa moja au kwa njia ya makampuni ya Kichina yameibuka barani tangu mfuko huu wa fedha ulipotangazwa.
Kipindi cha utekelezaji wa miradi
Serikali ya China yenye makao yake jijini Beijing, imekuwa ikisisitiza kuwa mwaka wa 2018 ni muhimu katika kalenda ya utekelezaji wa mpango huo. Hii kwa kiwango fulani, ndio sababu China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa FOCAC mwaka huu. Maafisa wakuu kutoka pande zote mbili wanakubaliana kwamba mkutano huo utatumika kutathmini mafanikio yaliyopatikana tangu 2015.
Kwa hiyo, ziara ya Wang Yi, kwa mujibu wa msemaji katika wizara ya mambo ya nje ya China, ni muhimu mno kwani inafuatilia mapendekezo na makubaliano ya ushirikiano zilizotiwa saini hivi karibuni kati ya China na nchi hizo tano.
Itakumbukwa kwamba Wang alikuwa kwenye ziara kama hiyo mwaka jana wakati alipotembelea Madagascar, Zambia, Tanzania, Congo, na Nigeria. Mwaka wa 2016 kiongozi huyo wa ngazi ya juu nchini China alizuru Namibia, Malawi, Mauritius, na Msumbiji. Katika mwaka wa 2015, Wang Yi alianza ziara yake ya Afrika kutoka Kenya kabla ya kuelekea Cameroon, Equatorial Guinea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan.
Baada tu ya kila ziara aliofanya, waziri huyo wa mambo ya nje amekuwa akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo, akisisitiza kwamba si utaratibu tu wa kawaida.
"Sisi siku zote tunasimama kwa pamoja na nchi zinazoendelea, na ndugu wa Afrika, kwa sababu nchi zinazoendelea ni msingi wa diplomasia ya China, na Afrika ni kiini cha msingi huu." Wang Yi aliwaambia waandishi wa habari nchini Nigeria mwaka jana baada ya ziara kama hiyo.
Akijibu maswali hasa kuhusu ajenda ya msingi wa nchi yake katika bara la Afrika, Wang Yi alidumisha kwamba China ina urafiki wa kweli na dhabiti pamoja na ushirikiano imara na Afrika. Kwa maoni yake, China ina nia na uwezo wa kuchangia katika amani na maendeleo ya Afrika kupitia kukuza ushirikiano na nchi za bara la Afrika.
"Tutaendelea kutekeleza sera ya uwazi katika ushirikiano wetu na Afrika, matokeo halisi, mshikamano na nia njema kama ilivyopendekezwa na Rais Xi Jinping, huku tukitekeleza matokeo ya mkutano wa Johannesburg na kuinua ushirikiano baina ya nchi mbalimbali kwa kuzingatia hali tofauti na mahitaji ya nchi za Afrika. "alibainisha
Ama kwa kweli China imethibitisha kuwa mfano wa kuigwa katika suala la kutimiza ahadi kwa kupitia hatua madhubuti ambayo matokeo yake yamedhihiri katika bara zima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |