China itaendelea kutoa mchango kwa ajili ya kushinda mapambano dhidi ya COVID-19
2021-05-10 19:33:39| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhimiza upatikanaji wa usawa wa chanjo ya virusi vya Corona katika nchi zinazoendelea, na kutoa mchango kwa ajili ya binadamu kushinda mapambano dhdi ya virusi hivyo.

Bibi Hua Chunying amesema, mkurugenzi mkuu wa WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema, Shirika hilo limeidhinisha chanjo ya Kampuni ya China ya Sinopharm kuwa ni salama, yenye ufanisi na sifa ya juu. Amesema, China imetangaza kutoa dozi milioni 10 ya chanjo kwa COVAX, ili zisambazwe kwa nchi zinazoendelea zenye mahitaji ya haraka.

Habari zinasema, chanjo ya COVID-19 ya Kampuni ya Sinopharm imeorodheshwa kwenye orodha ya chanjo kwa matumizi ya dharura ya WHO, ambayo ni chanjo ya kwanza iliyotengenezwa nje ya nchi za magharibi katika orodha hiyo.