Kundi la Taliban latangaza kusimamisha mashambulizi kwa siku tatu wakati wa Sikukuu ya Eid
2021-05-10 16:19:23| cri

Kundi la Taliban limetangaza kusimamisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali ya Afghanistan kwa siku tatu wakati wa Sikukuu ya Eid.

Taarifa iliyotolewa na Kundi hilo imesema, viongozi wa kundi hilo wametoa uamuzi huo ili kuwawezesha Waafghanistan kusherehekea sikukuu hiyo kwa usalama, na kuongeza kuwa, kama likishambuliwa, litajibu shambulizi hilo kwa nguvu.

Taarifa hiyo pia imesema, wapiganaji wote wa kundi hilo hawatakiwi kuingia kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali na wanajeshi wa serikali, pia askari wa serikali hawaruhusiwi kuingia kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.