Mapigano kati ya polisi wa Israel na Wapalestina yatokea katika sehemu takatifu mjini Jerusalemu
2021-05-10 19:38:08| Cri

Polisi wa Israel na waumini wa Palestina wamepambana ndani ya sehemu ya hatari katika eneo takatifu lililoko Jerusalemu leo asubuhi, na kusababisha majeruhi kwa Wapalestina wengi.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi la Israel imesema, maelfu ya Wapalestina walifanya vurugu katika uwanja wa msikiti wa Al-Aqsa na kuwarushia mawe na vitu vingine askari polisi wa Israel.

Vyombo vya habari vya Palestina navyo vimeripoti kuwa askari polisi wa Israel waliwarushia mabomu ya machozi waandamanaji kutoka Palestina waliokuwa ndani ya uwanja wa msikiti huo.

Mapema leo, jeshi la polisi la Israel lilitangaza kuwa Wayahudi hawataruhusiwa kutembelea eneo hilo hii leo, uamuzi uliotolewa wakati mvutano mkali ukiongezeka kabla ya Siku ya Wayahudi wa Israel, inayoadhimishwa na wazalendo wa Israel kwa gwaride linalopita Mji wa Zamani wa Jerusalemu Mashariki.