Mkuu wa WHO asema ushirikiano ni chaguo pekee la kumaliza janga la COVID-19
2021-05-11 09:31:24| CRI

 

 

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Tedros Ghebreyesus, amesema badala ya ushindani na upinzani, chaguo pekee la kumaliza janga la COVID-19 ni ushirikiano wa dunia nzima.

Bw. Tedros amesema nchi mbalimbali duniani zikishindania rasilimali au ushawishi wa kisiasa, virusi vitapata ushindi. Amehimiza nchi zote zivichukulie virusi vya Corona kama adui wa pamoja.

Amesema katika nchi zenye chanjo ya kutosha, idadi za vifo na wagonjwa wenye maambukizi makali imepungua, na utafiti wa awali pia umethibitisha kuwa chanjo inaweza kupunguza maambukizi. Hata hivyo ameonya kuwa pengo la upatikanaji wa chanjo kati ya nchi tofauti ni changamoto kubwa zaidi.

Takwimu zilizotolewa na WHO zinaonesha kuwa, nchi zenye kipato cha juu na cha kati zimechukua asilimia 83 ya chanjo ya COVID-19, huku nchi nyingine zikiwa na asilimia 17 tu.