Iran yafanya mazungumzo na Saudi Arabia
2021-05-11 08:39:30| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amethibitisha kuwa Iran na Saudi Arabia zimefanya mazungumzo hivi karibuni kujadili uhusiano wa nchi mbili na masuala ya kikanda.

Msemaji huyo amesema kuondoa mvutano na kujenga uhusiano kuna manufaa kwa nchi hizo mbili na eneo la Ghuba kwa ujumla. Amesema Iran siku zote inakaribisha mazungumzo na Saudia kwenye ngazi yoyote, na hii sio sera mpya ya Iran.

Kabla ya hapo, ofisa wa wizara ya mambo ya nje ya Saudia alithibitisha kufanyika kwa mazungumzo hayo, yanayolenga kupunguza mvutano wa kikanda.