China yapata mafanikio makubwa katika mambo ya haki za kibinadamu
2021-05-11 09:07:40| CRI

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema wachina bilioni 1.4 hawasumbuliwi na vita, umaskini, njaa na magonjwa ya mlipuko, na hii inaonesha kuwa shughuli za haki za kibinadamu nchini China zimepata mafanikio makubwa.

Kwenye kongamano kuhusu kuondoa umaskini na shughuli za haki za binadamu lililofanyika tarehe 8 mjini Ningde mkoani Fujian, balozi wa Cuba nchini China Bw. Carlos Miguel Pereira alisema China ilipopambana na janga la COVID-19 pia ilitimiza lengo la kuondoa umaskini uliokithiri. Pia alisema katika miaka zaidi 60 iliyopita, Cuba imekuwa ikisumbuliwa na vizuizi kama mauaji ya kimbari kutoka Marekani, na ilipinga kulifanya suala la haki za binadamu kuwa la kisiasa, na kutumia vigezo viwili kwenye suala hilo.

Bibi Hua Chunying ameitaka Marekani iache na kusahihisha mara moja vitendo vyake vya makosa vya kulifanya suala la haki za binadamu kuwa nyenzo ya kisiasa na kutumia vigezo viwili kwenye suala hilo, na kufuta mara moja vikwazo na vizuizi vya upande mmoja dhidi ya nchi mbalimbali ikiwemo Cuba, na kusema haya ni matakwa yanayokubalika kimataifa.