Wagonjwa 26 wa Corona wafa kwa kukosa oksijeni katika jimbo la Goa, India
2021-05-12 09:16:56| CRI

Wagonjwa wasiopungua 26 wa virusi vya Corona katika hospitali moja ya kiserikali jimboni Goa nchini India wamefariki dunia jana Jumanne kutokana na kukosa hewa ya oksijeni.

Tukio hilo lilitokea katika hospitali tanzu ya Chuo cha Udaktari cha jimbo la Goa, ambayo inahitaji mitungi 1,200 ya oksijeni, lakini hadi sasa imepata mitungi 400 tu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa jana na Wizara ya Afya ya India, nchi hiyo imerekodi kesi mpya za maambukizi 329,942 na vifo vipya 3,876 ndani ya siku moja.