Watu tisa wauawa kwenye shambulizi la kufyatua risasi huko Kazan Russia
2021-05-12 09:06:18| CRI

Watu tisa wakiwemo watoto saba wameuawa jana Jumanne baada ya mtu mwenye bunduki kuwafyatulia risasi watu waliopo shuleni huko Kazan mji mkuu wa Jamhuri ya Tatarstan nchini Russia.

Akitoa taarifa hizo rais wa Tatarstan Rustam Minnikhanov amesema, wavulana wanne, wasichana watatu na mwalimu mmoja pamoja na mfanyakazi mmoja wa shule walipoteza maisha yao kwenye shambulizi hilo lililotokea katika shule ya No. 175. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la TASS, watu 21 wamelazwa wakiwemo watoto 18 na watu wazima watatu, ambapo kati yao wanane wako hali mahututi.

Jumla ya watoto 714 na wafanyakazi 70 wakiwemo walimu 52 walikuwa shuleni wakati mshambuliaji alipoingia shuleni kupitia lango kuu la jengo na kufyatua risasi papo hapo akiwa na bunduki iliyosajiliwa rasmi.