UM waongeza makadirio kuhusu ongezeko la uchumi duniani
2021-05-12 18:14:20| CRI

Shirika la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa jana limetoa ripoti ikisema kuwa, itaongeza makadirio kuhusu ongezeko la uchumi duniani kutoka asilimia 4.7 kuwa asilimia 5.4 kutokana na mwelekeo wa nguvu wa kufufuka kwa uchumi wa Marekani na China.

Ripoti ya mwaka 2021 kuhusu mwelekeo na makadirio ya uchumi wa dunia imerekebisha makadirio kuhusu ongezeko la uchumi wa China kuwa asilimia 8.2 kutoka asilimia 7.2, kuinua makadirio kuhusu ongezeko la uchumi wa Marekani kuwa asilimia 6.2 kutoka asilimia 3.4, na kupunguza makadirio ya ongezeko la uchumi katika eneo la Ulaya linalotumia sarafu ya Euro kuwa asilimia 4.2 kutoka asilimia 5.

Ripoti hiyo inasema, uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea utafufuka na kufikia kiwango cha kabla ya janga la COVID-19 hadi mwaka 2022 au mwaka 2023