Wahamiaji haramu 70 waokolewa pwani ya Malta
2021-05-12 09:17:39| CRI

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Malta imesema wahamiaji haramu wapatao 70 wameokolewa kwenye pwani ya kusini ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara hiyo, wahamiaji hao waliokolewa baada ya kutoa ishara ya kuomba msaada, na sasa wamewekwa karantini baada ya kupimwa virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa jana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, kuanzia Januari mosi hadi Mei 11, jumla ya wahamiaji haramu 621 wamekufa maji kwenye bahari ya Mediterranean, wakiwa njiani kutoka Afrika Kaskazini kuelekea Ulaya.