Rais wa Afghanistan akataa suluhisho la kijeshi la mgogoro na kuitisha makubaliano ya kisiasa
2021-05-13 19:40:02| Cri

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mgogoro unaoendelea nchini humo, na kuutaka uongozi wa Taliban kuacha kupambana na kuunga mkono mchakato wa amani na kutafuta suluhisho la kisiasa.

Akizungumza baada ya swala ya Eid hii leo, rais Ghani amesema watu wa Afghanistan wanataka amani na kuvumiliana, na kutoa wito wa kuacha mapigano na mashambulizi ya mabomu, na badala yake kuunganisha juhudi zao pamoja na kujenga upya nchi hiyo.

Juhudi za kimataifa zinaendelea ili kupata suluhisho la mgogoro wa Afghanistan, ambao ulisitishwa miezi kadhaa iliyopita mjini Doha, na pendekezo la mkutano wa amani la Uturuki limeahirishwa tangu Machi kutokana na kundi la Taliba kutokuwa tayari kuhudhuria mkutano huo.