Rais wa Iran asema vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran ni “ukandamizaji dhidi ya maskini wa Iran”
2021-05-13 09:28:05| cri

 

 

Rais Hassan Rouhani wa Iran jana kwenye mkutano wa baraza la mawaziri amesema, vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran vimesababisha kupanda kwa bei za bidhaa na ukosefu wa dawa nchini humo, ambavyo ni “ukandamizaji dhidi ya maskini wa Iran na kukiuka haki za binadamu za wagonjwa wa Iran.”

Rais Rouhani amesema, ili kukabiliana na “vita vya kiuchumi” vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya Iran, wananchi wa Iran wameonesha ustahimilivu wao, na wanashinda vikwazo. Ameongeza kuwa kutokana na kufanyika kwa mkutano wa pande zilizosaini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA huko Vienna, “ukuta wa juu wa vikwazo unaanguka hatua kwa hatua.”