China yazindua idara ya kitaifa ya kuzuia na kudhibiti magonjwa
2021-05-13 16:55:45| Cri

China leo imezindua idara mpya ya kuzuia na kudhibiti magonjwa, ikiwa na kazi kuu tano ikiwemo kutunga sera za kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza.

Kuanzishwa kwa idara hiyo kunaashiria kupanuka kwa majukumu ya mamlaka za kudhibiti na kuzuia magonjwa, kutoka kuzuia na kudhibiti magonjwa mpaka kulinda kwa kina na kuboresha afya ya watu wote.

Taarifa rasmi imesema, mamlaka hiyo ni ya ngazi ya wizara ndogo na unasimamia na Kamati ya Afya ya Taifa, na itakuwa na kazi ya kuongoza maendeleo ya mfumo wa kuzuia na kudhibiti magonjwa, kufuatilia mlipuko wa magonjwa na mfumo wa kutoa tahadhari mapema, pia kutumia mfumo wa utafiti wa kisayansi katika kudhibiti magonjwa.