Tukio kuhusu Xinjiang lililoandaliwa na Marekani na wengine ni kichekesho
2021-05-13 08:54:53| CRI

Msemaji wa ujumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa mataifa  amekosoa vikali mkutano wa pembeni wa kilichoitwa hali ya haki za binadamu Xinjiang ulioandaliwa na Marekani, Uingereza, Ujerumani, pamoja na nchi nyingine na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Msemaji huyo amesema mkutano huo ulijaa uongo na mchezo mwingine wa ovyo wa Marekani na nchi chache, kujaribu kutumia suala la Xinjiang kuyumbisha China na kuidhibiti China. Amesema mkutano huo umepingwa na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa mataifa, ni upotoshaji na ni maonyesho mabaya ya kisiasa.

Amesema walioshiriki kuandaa mkutano huo wamepuuza hali halisi ya haki za binadamu mkoani Xinjiang, kwani kati ya mwaka 1990 na 2016 maelfu ya mashambulizi ya kigaidi yalitokea mkoani Xinjiang na kusababisha mamia ya vifo na maelfu ya majeruhi.

Amesema shutuma kuhusu mauaji ya kimbari, ajira ya kutumikisha, ubakaji na mateso vyote ni uongo, na mauaji ya kimbari ni kosa kubwa sana la kimataifa na neno hilo halitakiwi kutumiwa ovyo.