Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema Iran iko tayari kujenga uhusiano wa karibu na Saudia
2021-05-13 08:59:11| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif amesema Iran iko tayari kujenga uhusiano wa karibu na Saudi Arabia.

Bw. Zarif ambaye yuko ziarani nchini Syria amesema hayo baada ya kukutana na rais Bashar al-Assad wa Syria na mwenzake Faisal Al-Miqdad. Amesema Iran imefanya mawasiliano na Saudia, na kutumai kuwa mawasiliano hayo yatasaidia nchi hizo mbili kuimarisha ushirikiano ili kutimiza utulivu wa kikanda. Syria imeeleza kukaribisha ushirikiano kati ya nchi za kiarabu.