China yaihimiza Marekani ieleze wazi shughuli zake za kibaolojia za kijeshi ndani na nje ya nchi
2021-05-13 09:28:45| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Hua Chunying ameihimiza tena Marekani itoe maelezo kamili kuhusu shughuli zake za kibaolojia za kijeshi ndani na nje ya nchi, na kuchukua hatua ili kuhakikisha maabara zake za kibaolojia na shughuli husika ni halali, wazi na salama.

Bi. Hua amesema huu ni ufuatiliaji wa pamoja wa nchi nyingi. Amesema hivi karibuni Marekani ilitoa ripoti ya udhibiti wa silaha ikisema, shughuli zake zote zinaendana na Makubaliano ya kupiga marufuku silaha za kibaolojia, lakini haikutaja hata kidogo kituo cha kijeshi cha Fort Detrick kinachofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa.