China yaunga mkono waraka kuhusu kuondoa hakimiliki za ujuzi wa vifaa vya kinga na udhibiti wa COVID-19 kuingia kipindi cha kujadiliwa
2021-05-13 19:59:17| CRI

Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo hapa Beijing amesema, China ni nchi ya kwanza kupendekeza na kutekeleza kuifanya chanjo ya virusi vya Corona kuwa bidhaa ya umma ya afya duniani.

Amesema China inaunga mkono waraka kuhusu kuondoa hakimiliki za ujuzi wa vifaa vya kinga na udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo kuingia kwenye kipindi cha kujadiliwa. Ameongeza kuwa, katika hatua ifuatayo, China itashirikiana na pande mbalimbali katika majadiliano, na kuhimiza kufikia utatuzi wenye uwiano na ufanisi, ili kuzifanya nchi mbalimbali zitokomeze virusi vya Corona haraka iwezekanavyo.

Hivi sasa nchi wanachama wa WTO zinajadiliana juu ya suala la kupatikana kwa chanjo ya COVID-19 duniani.