China sasa yahitaji vipimo viwili hasi kumaliza karantini inayotokana na COVID-19
2021-05-14 19:04:13| CRI

 

Mwongozo uliotolewa na kikosi kazi cha kukabiliana na virusi vya Corona kilicho chini ya Baraza la Serikali la China umesema, abiria wanaowasili nchini humo na watu waliowasiliana kwa karibu na watu walioambukizwa virusi vya Corona wanaweza kuruhusiwa kutoka kwenye karantini kama vipimo viwili tofauti vya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwenye koo na pua havitakutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Mwongozo huo umesema, kimsingi, vipimo hivyo viwili vinavyofanywa wakati watu hao wakiwa karantini na wanaporuhusiwa kutoka karantini, vinapaswa kutumia vitendanishi viwili tofauti kwa sampuli hizo mbili tofauti.

Mwongozo huo pia umesema, watu wanaoruhusiwa kutoka karantini wanapaswa kufanya vipimo siku ya pili na ya saba baada ya uchunguzi wa kidaktari kumalizika, na wanatakiwa kufuatilia kwa karibu afya zao na kuepuka mikusanyiko.