Utafiti waonyesha udhibiti wa janga la COVID-19 waongeza imani ya wananchi wa China kwa serikali yao
2021-05-14 17:06:06| CRI

 

 

Utafiti uliochapishwa kwenye gazeti la Washington Post la nchini Marekani umeonyesha kuwa, hatua zilizochukuliwa na serikali ya China katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona zimeongeza imani ya wananchi na kuridhishwa na utendaji wa serikali hiyo.

Profesa wa sosiolojia katika Chuo Kikuu cha York nchini Canada, Cary Wu, kwa kushirikiana na wasomi wengine 17 wa China waliandikisha zaidi ya wanafunzi 600 kutoka vyuo vikuu 53. Wasomi hao walifanya utafiti mwishoni mwa mwezi April mwaka jana kupitia mahojiano ya moja kwa moja kwa njia ya mtandao na watu 19,816 kutoka mikoa 31 ama miji yeny hadhi ya mikoa nchini China.

Utafiti huo uligundua kuwa, imani ya Wachina kwa serikali kuu ilifikia asilimia 98, huku imani yao kwa serikali za mitaa pia ikifikia asilimia 91. Pia utafiti huo uligundua kuwa, asilimia 49 ya wahojiwa wameongeza zaidi imani yao kwa serikali tangu janga hili lilipotokea, asilimia 48 hawakuona mabadiliko yoyote, na asilimia 3 tu ndio walikosa imani na serikali.