Rais Joe Biden asema shambulizi la udukuzi dhidi ya bomba la nishati la Marekani halihusiani na serikali ya Russia
2021-05-14 09:33:57| cri

 

 

Rais Joe Biden wa Marekani amesema tukio la shambulizi lililofanywa na wadukuzi dhidi ya bomba la kusafirisha mafuta la kampuni ya Colonial Pipeline halihusiani na serikali ya Russia, lakini anatarajia kukutana na rais Vladimir Putin wa Russia na kufanya naye mazungumzo kuhusu suala la uhalifu wa mtandaoni.

Siku hiyo rais Biden amesema, Marekani haioni kuwa serikali ya Russia inahusika na shambulizi hilo, lakini ina imani kuwa washambuliaji wanaishi nchini Russia.

Rais Biden amesema nchi zinazowajibika lazima zichukue hatua dhidi ya uhalifu wa mtandaoni, na Marekani inajaribu kuweka vigezo husika vya kimataifa.