Safari za ndege za abiria za ndani nchini China zaongezeka kwa mara tatu mwezi Aprili
2021-05-14 19:38:56| CRI

Mamlaka ya Usafiri wa anga nchini China leo imesema, idadi ya safari za ndege za ndani za abiria nchini humo zimefikia milioni 51.09 katika mwezi Aprili, ambayo imeongezeka kwa asilimia 205.5 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Idadi hiyo imeweka rekodi mpya ya mwezi kuanzia mwaka 2020, sawa na asilimia 96.2 ya idadi hiyo kwa mwaka 2019 wakati kama huo.

Usafirishaji wa mizigo na barua umefikia tani laki 6.55, ikiongezeka kwa asilimia 35 kuliko mwaka jana wakati kama huo.