Rais Xi Jinping wa China akagua mradi wa usafirishaji maji
2021-05-14 09:35:34| Cri

Rais Xi Jinping wa China amekagua Mradi wa Usafirishaji Maji kutoka Kusini hadi Kaskazini katika mji wa Nanyang katikati mwa Mkoa wa Henan nchini China.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Machi, mradi huo umesafirisha zaidi ya mita za ujazo bilioni 40.8 za maji kwenye maeneo yenye ukame yaliyoko kaskazini mwa China, na watu zaidi ya milioni 130 wamenufaika moja kwa moja na mradi huo tangu kipindi cha kwanza cha mradi huo katika sehemu za mashariki na kati kilipoanza kusafirisha maji.