Bomba kuu la mafuta nchini Marekani larejesha huduma baada ya kufungwa kutokana na shambulizi la udukuzi
2021-05-14 08:57:47| CRI

Bomba kuu la kusafirisha mafuta nchini Marekani limerejesha huduma baada ya kufungwa kwa siku sita kutokana na shambulizi la udukuzi.

Kampuni ya Colonial Pipeline inayoendesha bomba hilo linalosambaza mafuta ya petroli na dizeli kwenye sehemu za mashariki na kusini mashariki za Marekani, imesema mfumo mzima wa bomba hilo umewashwa upya, na itachukua siku kadhaa kabla ya mnyororo wa ugavi kurudi kwenye hali ya kawaida.