Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Bibi Henrietta Fore, ametoa taarifa kuhimiza Kundi la G7 kutoa chanjo ya COVID-19 kwa mpango wa COVAX ili kutatua ukosefu wa chanjo wa mpango huo.
Bibi Fore amesema kundi hilo na Umoja wa Ulaya ukitoa asilimia 20 ya utengenezaji wa chanjo kwa mwezi wa Juni, Julai na Agosti, itaweza kutoa dozi milioni 153 kwa mpango huo. Idadi hiyo haitaathiri mpango wao wa ndani.
Habari zinasema kutokana na hali mbaya ya janga la COVID-19 nchini India ambayo ni nchi muhimu inayotengenza chanjo, mpango wa COVAX utakuwa na ukosefu wa dozi milioni 140 za chanjo ambazo zimepangwa kutumiwa katika nchi zenye mapato ya kati na ya chini mwishoni mwa mwezi huo.