Zaidi ya dozi milioni 400 za chanjo ya COVID-19 zatolewa nchini China
2021-05-17 18:39:23| CRI

 

 

Kamati ya afya ya taifa ya China imesema hadi kufikia Jumapili zaidi ya dozi milioni 406.9 za chanjo ya COVID-19 zimetolewa nchini China wakati juhudi za kutoka chanjo zikielendea.

China inaendelea na juhudi za utoaji chanjo wakati hivi karibuni kumekuwa na watu saba waliokumbwa na maambukizi ndani ya jamii katika mkoa wa Anhui, na wengine tisa katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Liaoning. Mikoa yote imeongeza hatua za ufuatiliaji wa watu waliokaribiana na wale walioambukizwa na upimaji.