Mkuu wa UM azihimiza Palestina na Israel zisitishe uhasama mara moja
2021-05-17 09:44:01| cri

 

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana kwenye mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu mgogoro kati ya Palestina na Israel, amezihimiza pande hizo mbili zisitishe uhasama mara moja.

Bw. Guterres amesema, huenda mgogoro huo utaleta maafa kwa wananchi wa nchi hizo mbili na kanda nzima, na kwamba pande mbalimbali lazima zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa na sheria ya haki za kibinadamu.

Ameongeza kuwa, hali ya hivi sasa ya Jerusalem lazima ilindwe na kuheshimiwa, na kusisitiza kuwa, kurudi kwenye mazungumzo ni njia ya pekee ya kumaliza mvutano kati ya pande hizo.