Kampeni za urais zaanza Syria
2021-05-17 08:55:47| CRI

Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Syria zimeanza rasmi jana Jumapili.

Chini ya kaulimbiu ya “Matumaini Yako Kazini”, rais wa sasa Bashar al-Assad ameanza kampeni yake mjini Damascus na katika mikoa mingine.

Uchaguzi huo utafanyika Mei 20 kwa raia wa Syria walioko nje ya nchi na Mei 26 kwa wasyria walioko nchini humo.